Hawa Ndio Wasanii Walipo Chini Ya Label Ya AliKiba ‘ Kings Music Label’

Alikiba amweza kuwa gumzo sana wiki hii na hii ni baada ya kibao chake kipya kwa jina HELA kupotea katika mtandao wa Youtube ila baadae inabainika wazi kuwa imefutwa na hii labda ni baada ya washabiki waliotazama kibao hicho waliweza kuiponda kwa sana na kudai msanii kama kiba anafaa kutoa vibao vikali zaidi.

Ali Kiba Ataja Sababu Ya Kufuta Nyimbo Yake

 

Baada Ya gumzo la Kutolewa kwa kibao chaki Kiba kwa sasa ameamua kutambulisha rasmi wasanii waliopo Chini ya Kings Music Label kando na yeye na Abdukiba, wakiwa ni Killy amabe tayari anafahamika kwa kiwango flani  apo awali katika mziki wa bongo fleva wakati alikua chini ya Uongozi wa Aljazeera Enterainment  ila wengine wageni kwenye game ni K2GA na Rashid.

Alikiba na Wasanii Walipo Chini Ya Kings Music Label

 

Kufikia Sasa Alikiba Ameweka wazi anwasaidia wasanii hao baada tu ya  kuachia video ya wimbo mpya unaokwenda kwa jina la ‘Mwambie Sina’ akiwa na kundi lake  la King’s Music Records, Alikiba amesema kuwa ni muda wa kurudisha kwa jamii kwa kusaidia kukuza sanaa.

Msanii huyo wa muziki nchini Tanzania, Kiba amesema hayo kupitia kwa mitandao yake ya kijamii ya Twitter na Instagram.

”Sasa ni wakati rasmi wa kurudisha kwa jamii kwa kusaidia kukuza sanaa kwa kutambulisha na kuvipa support vipaji vipya kwa industry. Nawatambulisha kwenu vijana wangu Cheed, Killy, K2ga na Abdukiba kutoka record label yangu King’sMusic,” amesema Alikiba.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *