Wema Sepetu Akana Kutoka Na Dogo Janja Na Kutambulisha Mpenzi Mpya

Tanzanian Sweet heart , Wema Sepetu amekanusha vikali tetesi ambazo ziliibuliwa na mwanaharakati wa mitandao ya kijamii Mange Kimambi kwamba kuna siku alichepuka na Dogo Janja amabae ni mume wa kisheria wa mlimbwende/mwanamitindo Irene Uwoya..

Mange Kimambi ambaye amekuwa akilumbana kwenye mitandao ya kijamii na Wema Sepetu kwa mda mrefu sasa siku ya jana alipost chart mtandaoni akionyesha mazungumzo yake na Dogo Janja kuhusiana na tetesi hizo.

mseto wa hisia ulizuka katika kurasa za mange kumfanya afikie kufuta ujumbe huo muda mchache baada ya kuchapisha , ilisababisha watu wengi mtandaoni kudai kwamba taarifa hizo hazikuwa na ukweli wowote.

Baada ya kuibuka kwa  tetesi hizo, Wema ametumia mtandao wa Insta siku ya jana kumtangaza mpenzi wake mpya, amedai sio kweli kwamba anatoka kimapenzi na mpenzi huyo wa Irene Umoya.

“Pale unapoona mtu anakuongelea vitu visivyo make sense ili mradi tu… Mi Arusha nimeenda Lini…??? Na Huyo Dogo nimekaa nae WAPI…???? Hata mazoea nae sina…!!!Ila Dada anakuwaga na stress za ajabu sometimes… Kimambi… Utaniacha lini nipumue in Peace…!??? You are Obsessed wallahy,” aliandika Wema Sepetu.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *