“Hii niatua kubwa sana na mtihani unamkuta kila binadamu na mwenye kuutatua ni Mungu mwenyewe niwashukuru wote mlioweza kumuombea dua Hawa mpaka apa alipo na pia niendelee kuwaomba msiache kuomba dua @diamondplatnumz mdogowangu napenda sana unavyokua na roho ya kutoa ila kaa ukijua hii umeweka na Mungu atakupa kwa njia nyingine.

Leo acha niseme tu huyu dada Speedy Recovery International Health Care Services ametusaidia na nikikwambia nimemjulia tu kupitia instagram na alikua ananiambia anauzoefu wa miaka 32 kwenye kazi ya udakitari niliona kama anataka kuniibia tu ila mwisho wa siku ndiye aliyesaidia kila kitu na ajaniomba hata mia hii yote ni mipango ya Mungu kulifanya jambo kua jepesi. Naomba niombeeni ruhusa kwa @sallam_sk na @mkubwafellatmk nirudi dar maana nimesha maliza walichonituma ili niweze kuwahi Wasafi festival,” Aliandika Babu Tale