KUTANA NA RAJAB RASHID NYOTA ANAYENG’ARA KUPITIA TAMTHILIA YA MAZA!

Katika ulingo wa michezo ama sanaa na wasanii wa kucheza uigo wa tamthilia kwenye filamu, ambao wengi huburudishwa kwa zamu kila uchao ndani ya sebule zao na wasanii hawa, leo ninakusogezea karibu na mmoja ya wasanii hawa maarufu kama Rajab Rashid ambaye anafamika kwa jina la mchezo wa Maza kama Safari. Kwanza kwa wale mashabiki wa Maza, ambapo kipindi hiki kinarushwa hewani kupitia Maisha Magic East kuanzia siku ya Jumatatu hadi Ijumaa saa moja na nusu, ambao wamehinikiza kote katika eneo zima la Africa Masharaiki na eneo la maziwa makuu yani ikiwemo Burundi hadi Congo.

Safari akiwa kwenye ubora wake.

Rajab Rashid nikati ya wasanii wachanga na wanao panda kwa kasi sana kwenye ulimbwende huu wa sanaa ya uigizaji, na amejizolea wafuasi wengi kwa mda mfupi tu kwa jinsi anavyoibugia na kuiwakilisha sanaa yake ya kuiga ama uigizaji. Wengi wanamtambua kama Safari katika tamthilia ya Maza, anapoiga kama kijana bawabu anayefanyia kazi kwenye kasri la watu wenye uwezo wa mali. Lakini je ilikuaje hadi nyota huyu akajikuta katika harakati ya kuiga kwenye tamathilia kubwa kama hii inayopaa kimataifa?

Safari kabla ya kujiunga na tamthilia ya Maza, hapa akiiga kwenye mchezo wa kuiguiza kama askari ndani ya Shirika la Kwacha Afrika.

Akizungumza kupitia meza yetu ya habari ya Y254 tv kupitia wovuti wetu wa habari za burudani ya Chitchat, Rajab ansema alishawahi kuwa chini ya shirika lisilio la kiserekali kwa jina Kwacha Afrika. Shirika la Kwacha Africa liliundwa na vijana mwanzoni mwa mwaka wa 2000, kwaniaba ya kuelimisha jamii kupitia sanaa ya uigizaji. Na tokea hapo limekua likishughulika kwa sana katika kukuza vipaji vya wasanii kama Rajab. Kwahivyo kupitia shirika hili, na kwa bidii aliyokua nayo ya uigizaji, nyota huyu wa tamthilia ya Maza alijikuta kapata nafasi ya kuingia kwenye majaribio ya uigizaji kwenye televisheni ambapo alifanikiwa kujumlishwa na alipata fursa ya kuiga kama Safari. Kitu ambacho kilimfanya kufanikiwa kujiunga kufanyia kazi talanta yake ndani ya tamthilia hii ya Maza ni heshima, busara na uvumilivu alionao.

Safari akiwa kwenye muigo na msanii mwenzake ndani ya tamthilia ya Maza.

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *