MFAHAMU ZAIDI DIWANI NZARO LEJENDARI WA MUZIKI NDANI MAROON COMMANDOS!

 

Diwani Nzaro Lewa

 

Muziki ni tija ya kipekee inayowakosha na kuwaongoa maelfu kwa   mamilioni ya mashabiki duniani, chambilicho alivyoimba mwanamuziki mukongwe wa muziki wa rhumba kutokea Tanzania hayati Marijani Rajab kwenye kibao chake maarufu kwa jina ”Muziki”. Basi shabiki wangu je unalifahamu kundi maarufu la muziki hapa nchini la Maroon Commandos, ambalo linajumuisha bandi ya muziki ya kikosi cha kijeshi cha 7 battalioni  (Kenya Army Infantry) cha jeshi la nchi kavu? Kutokana na ukwasi wao na wepesi wa kuimba nyimbo tamu zilizo vuma duniani kama vile Riziki haivutwi, Dawa nimuone  hani, Shikamoo na nyingine nyingi zilizoundwa kwenye mifumo ya Rhumba, Benga na mifumo mingi mingineo. Ndio maana leomwandishi wako Changez Ndzai nimepata fursa na nimeingia ndani kabisa kwenye kambi ya kijeshi iliyopo maeneo ya Lang’ata maarufu kama Lang’ata Barack , nakumusaka mmoja ya wanamuziki na mwanajeshi ambaye pia mbali na kuwa ndani ya kikosi hiki anajishughulisha na uongozi wa kundi lake mwenyewe la muziki ambalo limefanikiwa kutoa vibao vitamu kama, Nihendedze, Hamtaweza, Msiwabake navingine vingi tu.

 

Diwani Nzaro akifanya yake.

Diwani Nzaro Lewa, amekuwa katika mstari wambele sana katika kuhakikisha muziki wa asili unavuma pia haswa kwakutukia lugha ya Giriama. Msanii huyu ambaye pia kila sherehe zote za kiserekali zinapofanyika, huweza kupewa fursa kutumbuiza mashabiki wake kupitia bandi yake. Mbali na sherehe za Kiserekali, Diwani pia huhusika sana kutumbuiza katika kumbi mbalimbali za sanaa na mbali na kuingisha kipato chake kwa kupitia kazi ya uanajeshi basi muziki umekua ni kitega uchumi mbadala kwake huku nyimbo zake pia zikidukuzwa na kuuzwa kwenye mitandao mbalimbali ya uzaji bidhaa kama vile Amazon. Chini hapa ni baadhi  ya picha zake akiwa katika harakati zake za kutumbuiza umma kupitia bandi yake ya muziki.

 

 

 

Leave a Reply

Your email address will not be published. Required fields are marked *